Posts

171 - Hukumu

 171 - Hukumu "The Judgement Has Set" 1. Imeanzishwa hukumu mbinguni; tutasimamaje pale; Apimapo Mungu Hakimu kila wazo na tendo? Tutasimamaje sote katika siku kuu ile? Dhambi zetu zitafutika ama zitatuangusha? 2 Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai; Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu. 3 Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja, Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie! (Amina)

172 - Mfalme Ajapo

  172 - Mfalme Ajapo "I Called To The Feast" 1. Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;  Itakuwaje nasi kule Bwana ajapo? Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!  Itakuwaje na sisi, Bwana akija? 2. Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba;  Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo. 3. Kwa furaha awakubali wenye mavazi ya arusi;  Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo. 4. Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;  Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo! 5. Mfalme utupe neema sisi tunapokungoja,  Tusiogope kukuona ujapo Bwana. (Amina)

173 - Hatujui Saa

173 - Hatujui Saa "We Know Not The Hour" 1. Hatujui sa-a ya kuja kwa Bwana, Lakini dalili zasema karibu, Atakaporudi, -lakini kwa kweli, Hatujui sa-a. Atakuja, kwa vile tukeshe; Atakuja Mwokozi, Aleluya! Atakuja kwa fahari ya Baba yake, -Hatujui saa. 2. Pana nuru kwao wapendao haki, Pana kweli katika Chuo Cha Mungu; Unabii hufundisha kuja kwake, -Hatujui saa. 3. Tutakesha tutaomba daima, Tutafanya kazi mpaka akija; Tutaimba na tutasoma ishara, -Hatujui saa.   (Amina)

174 - Tukimgojea

  174 - Tukimgojea "We Know Not The Time When He Cometh" 1. Sijui atakapokuja, Mchana au usiku; Labda sa-a ya alasiri. Pengine ni alfajiri. Hutwambia tuwe tayari, Ta-a zetu tusizime;  Ili ajapo atukute; Tuwe tukimngoja Yeye.  Tu---kimngoje---a,   (Kukesha, tunakungoja Wewe)  Tu---kimngoja---a,   (Kukesha, tunakungoja Wewe)  Tu---kimngoja---a,   (Kukesha, tunakungoja Wewe)  Twakesha, twamngoja Yeye . 2. Nakumbuka huruma zake, Bei ya wokovu wetu;  Aliacha nyumba tukufu Awafilie wabaya. Ninadhani itampendeza, Kama sisi watu wake,  Tukionyesha pendo letu, Tuwe tukimngoja Yeye.  3. Ee Yesu, Mwokozi mpendwa, Wajua nalihifadhi  Tumaini la kukuona. La kukaribishwa nawe. Ukija kwa watu wengine, Kama mhukumu wao,  Kwangu utakuwa rafiki, Nakesha, nakungojea.    (Amina)

175 - Uso Kwa Uso

175 - Uso Kwa Uso "Face To Face" 1. Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;  Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;  Na kwa utukufu wake  nitamwona milele. 2. Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa,  Bali atakapokuja, nitamwona halisi. 3. Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;  Kipotovu kitanyoshwa, fumbo  litafumbuka. 4. Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;  Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.    (Amina)

176 - Ati Tuonane Mtoni?

176 - Ati Tuonane Mtoni? "Shall We Gather At The River" 1. Ati tuonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu;  Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu. Naam, tuonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!  Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu. 2. Tukitembea mtoni na Yesu Mchunga wetu, Daima tu ibadani usoni pake kwetu. 3. Tukisafiri mtoni tutue ulemeao Wema wa Mungu yakini; una taji na yao! 4. Kwang`ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,  Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo. 5. Karibu sana mtoni, karibu tutawasili,  Mara huwa furahani na amani ya kweli.   (Amina)

177 - Kazi Yangu Ikiisha

 177 - Kazi Yangu Ikiisha "When My LIfe Work Is Ended" 1. Kazi yangu ikisha,nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua mwokozi nifikapo ng`amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki. Nitamjua,Nitamjua,nikimwona uso kwa uso; Nitamjua,Nitamjua,kwa alama za misumari. 2. Furaha nitapata nikiona makao` Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu Mwokozi kwa rehama na pendo; Vilivyonipa pahali mbinguni. 3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza. 4. Milangoni mwa mji Bwana atanipisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele;lakini Nataka kumwona mwokozi kwanza. (Amina)