Posts

Showing posts from April, 2023

171 - Hukumu

 171 - Hukumu "The Judgement Has Set" 1. Imeanzishwa hukumu mbinguni; tutasimamaje pale; Apimapo Mungu Hakimu kila wazo na tendo? Tutasimamaje sote katika siku kuu ile? Dhambi zetu zitafutika ama zitatuangusha? 2 Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai; Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu. 3 Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja, Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie! (Amina)

172 - Mfalme Ajapo

  172 - Mfalme Ajapo "I Called To The Feast" 1. Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;  Itakuwaje nasi kule Bwana ajapo? Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!  Itakuwaje na sisi, Bwana akija? 2. Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba;  Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo. 3. Kwa furaha awakubali wenye mavazi ya arusi;  Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo. 4. Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;  Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo! 5. Mfalme utupe neema sisi tunapokungoja,  Tusiogope kukuona ujapo Bwana. (Amina)

173 - Hatujui Saa

173 - Hatujui Saa "We Know Not The Hour" 1. Hatujui sa-a ya kuja kwa Bwana, Lakini dalili zasema karibu, Atakaporudi, -lakini kwa kweli, Hatujui sa-a. Atakuja, kwa vile tukeshe; Atakuja Mwokozi, Aleluya! Atakuja kwa fahari ya Baba yake, -Hatujui saa. 2. Pana nuru kwao wapendao haki, Pana kweli katika Chuo Cha Mungu; Unabii hufundisha kuja kwake, -Hatujui saa. 3. Tutakesha tutaomba daima, Tutafanya kazi mpaka akija; Tutaimba na tutasoma ishara, -Hatujui saa.   (Amina)

174 - Tukimgojea

  174 - Tukimgojea "We Know Not The Time When He Cometh" 1. Sijui atakapokuja, Mchana au usiku; Labda sa-a ya alasiri. Pengine ni alfajiri. Hutwambia tuwe tayari, Ta-a zetu tusizime;  Ili ajapo atukute; Tuwe tukimngoja Yeye.  Tu---kimngoje---a,   (Kukesha, tunakungoja Wewe)  Tu---kimngoja---a,   (Kukesha, tunakungoja Wewe)  Tu---kimngoja---a,   (Kukesha, tunakungoja Wewe)  Twakesha, twamngoja Yeye . 2. Nakumbuka huruma zake, Bei ya wokovu wetu;  Aliacha nyumba tukufu Awafilie wabaya. Ninadhani itampendeza, Kama sisi watu wake,  Tukionyesha pendo letu, Tuwe tukimngoja Yeye.  3. Ee Yesu, Mwokozi mpendwa, Wajua nalihifadhi  Tumaini la kukuona. La kukaribishwa nawe. Ukija kwa watu wengine, Kama mhukumu wao,  Kwangu utakuwa rafiki, Nakesha, nakungojea.    (Amina)

175 - Uso Kwa Uso

175 - Uso Kwa Uso "Face To Face" 1. Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;  Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;  Na kwa utukufu wake  nitamwona milele. 2. Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa,  Bali atakapokuja, nitamwona halisi. 3. Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;  Kipotovu kitanyoshwa, fumbo  litafumbuka. 4. Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;  Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.    (Amina)

176 - Ati Tuonane Mtoni?

176 - Ati Tuonane Mtoni? "Shall We Gather At The River" 1. Ati tuonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu;  Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu. Naam, tuonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!  Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu. 2. Tukitembea mtoni na Yesu Mchunga wetu, Daima tu ibadani usoni pake kwetu. 3. Tukisafiri mtoni tutue ulemeao Wema wa Mungu yakini; una taji na yao! 4. Kwang`ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,  Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo. 5. Karibu sana mtoni, karibu tutawasili,  Mara huwa furahani na amani ya kweli.   (Amina)

177 - Kazi Yangu Ikiisha

 177 - Kazi Yangu Ikiisha "When My LIfe Work Is Ended" 1. Kazi yangu ikisha,nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua mwokozi nifikapo ng`amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki. Nitamjua,Nitamjua,nikimwona uso kwa uso; Nitamjua,Nitamjua,kwa alama za misumari. 2. Furaha nitapata nikiona makao` Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu Mwokozi kwa rehama na pendo; Vilivyonipa pahali mbinguni. 3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza. 4. Milangoni mwa mji Bwana atanipisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele;lakini Nataka kumwona mwokozi kwanza. (Amina)

178 - Ukingoni Mwa Tordani

178 - Ukingoni Mwa Tordani "On Jordan" 1. Ukingoni mwa Yordani ninaangalia  Bara nzuri ya Kanaani, ninayotamani.  Tutakaa pamoja na Yesu, Katika pwani yenye raha;  Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo, Milele hata milele. 2. Bara ile ina nuru, nuru ya milele; Kristo, Jua, hutawala, hufukuza giza. 3. Nitapafikia lini na kubarikiwa, Penye ufalme wa Baba, na kumwona uso? 4. Furaha yangu rohoni ni  kuchukuliwa; Siyaogopi mawimbi katika Yordani. (Amina)

179 - Watafurahi

179 - Watafurahi "Joy By And By" 1. Wavunaji watafurahi, pale watakaporudi, Wakiyaleta mavuno hata Yerusalemu. Furaha wataipata, furaha hata milele, Furaha, wataipata, wakati wa mavuno. 2. Na siku ile tutaimba, kumshukuru na kumsifu, Bwana Yesu Jumbe wetu, kule Yerusalemu. 3. Wavunaji watafurahi makaoni mwa milele, Yaliyowekwa tayari kule Yerusalemi.   (Amina)

180 - Pana Mahali Pazuri Mno

180 - Pana Mahali Pazuri Mno "Sweet By And By" 1. Pana mahali pazuri mno, Twapaona kwa mbali sasa;  Baba yetu angoja pale, Amepanga makao yetu. Kitambo tu bado, Tutakutana ng`ambo pale.  Kitambo tu bado, Tutakutana ng`ambo pale. 2. Tutaimba pale kwa moyo Nyimbo tamu za wenye heri.  Na rohoni hatutaona Tena haja ya kupumzika. 3. Kwa baba yetu mkarimu Tutatoa shukrani sana.  Kwa kipaji cha pendo lake Na baraka anazotupa. (Amina)

181 - Tutakaa Mahali Pa Maji

181 - Tutakaa Mahali Pa Maji 1. Mahali pa maji mazuri maji ya uzima;  Anapotungoja Yesu tutakaribishwa. Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima;  Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima. 2. Tunapochoka safarini, tamu kupumzika.  Panapo maji ya uzima yatufurahisha. 3. Una kiu? Uje kwa Yesu, utaburudishwa;  Yesu yu maji ya uzima, unywe,uokoke.   (Amina)

182 - Hapana Giza

182 - Hapana Giza "No night There" 1. Mchana hauishi Mjini mzuri; Mji hautapita; Na hapana giza. Machozi yatafutwa, Kifo hapana pale;  Hawahesabu siku, Na hapana giza. 2. Milango ni ya lulu, Mjini mzuri; Dhahabu njia zake; Na hapana giza. 3. Milango haifungwi Mjini mzuri;  Mto ni wa uzima Na hapana giza. 4. Hawahitaji jua Mjini mzuri,  Mwana Kondoo nuru; Na hapana giza. (Amina)

183 - Yesu Anaporudi

183 - Yesu Anaporudi "There'll Be No Dark Valley" 1. Furaha na raha tutapata, Furaha na raha tutapata,  Furaha na raha tutapata Yesu anaporudi. Yesu anaporudi (rudi) Yesu anaporudi (rudi);  Furaha na raha tutapata Yesu anaporudi. 2. Tutaimba nyimbo za shangwe kuu, Tutaimba nyimbo za shangwe kuu,  Tutaimba nyimbo za shangwe kuu Yesu anaporudi. 3. Hapana machozi arudipo, Hapana machozi arudipo,  Hapana machozi arudipo, kwa wateule wake. (Amina)

184 - Panapo Pendo

184 - Panapo Pendo "Love At Home" 1. Vitu vyote ni sawa, panapo pendo: Kila sauti tamu, panapo pendo Pana amani pale, na furaha nyumbani, Siku zote salama panapo pendo. Panapo upendo - Siku zote salama Panapo pendo. 2. Furaha I nyumbani, panapo pendo: Hapana machukizo, panapo pendo; Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi, Maisha ni kamili, panapo pendo. 3. Hata mbinguni juu, pana furaha Wakiona upendo nyumbani mwetu. Macho yapendezwa na viumbe vya Mungu, Naye Mungu huona, panapo pendo. 4. Ee Yesu niwe wako, wako kabisa, Ndipo patakuwako Pendo nyumbani; Nitakaa salama, sitafanya dhambi: Nitabarikiwa tu panapo pendo. (Amina)

185 - Mungu, Mapenzi Makamilifu

185 - Mungu, Mapenzi  Makamilifu "O Perfect Love" 1. Mungu u mapenzi mtakatifu Yapitayo fahamu za watu  Twanyenyekea sisi wapungufu, Wape baraka wapenzi wetu. 2. Ewe Mapenzi yasiyopimika Twawaombea kitini Mwako,  Wape mapenzi yasiyotindika, Waliooana mbele yako. 3. Ewe uhai, wewe u dhamana Ya imani na matumaini,  Wape kuvumilia hapa sana  Wasiche maumivu mwishoni. 4. Wape furaha hiyo iwezayo kutia nuru kwenye huzuni,  Wape amani hiyo itakwayo Katika matata duniani. 5. Waende mbele kusaidiana Maisha yao ulimwenguni;  Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, Wafurahi milele mbinguni. (Amina)

186 - Hatutaagana Tena

  186 - Hatutaagana Tena "With Friends On Earth" 1. Tuonanapo na rafiki sote twafurahi,  Ila tumepaswa mwishowe kuagana tena. Hatutaagana tena nyumbani mbinguni,  Kwenye nchi tamu juu, Hatutaagana. 2. Twatumaini kwa furaha tutaonana juu  Na rafiki tulioaga tuishapo shinda. 3. Kule hatutatamka kamwe neno la kuaga,  Tutaimba daima tena nyimbo za furaha. (Amina)

187 - Kufariki Naye Yesu

187 - Kufariki Naye Yesu "Asleep In Jesus" 1. Kufariki naye Yesu! Usingizi wewe heri;  Raha isiyofujika kwa majozi na adui. 2. Kufariki naye Yesu! Lo! Ya kubwaga simanzi  Na kulala na amani hata Bwana awatuze. 3. Kufariki naye Yesu! Heri watakaoamshwa,  Wataona siku ile utukufu wake Bwana. 4. Kufariki naye Yesu! Wataamka aitapo;  Watapasua kaburi na kutoka watukufu.   (Amina)

188 - Wimbi Litakasalo

188 - Wimbi Litakasalo "The Cleansing Wave" 1. Wimbi la damu ya Yesu Linatutakasa;  Aliumia kusudi Tupate uzima. Wimbi la damu naona, Naingia, natakaswa!  Bwana asifiwe sana, Hutakasa, hutakasa. 2. Damu inasema kwangu, Nasikia mvuto;  Inasema, moyo wangu Hutakaswa nayo. 3. Naondoka kutembea Kwa nuru ya mbingu;  Mavazi yamesafishwa; Moyoni ni Yesu. 4. Neema ni ya ajabu, Kutakaswa ndani!  Na kuwa naye Yesu tu, Aliye Mwokozi. (Amina)

189 - Tubatize upya

189 - Tubatize upya "Baptize Us A New" 1. Mimina upya nguvu toka juu;  Tupe pendo lako, ewe Mwokozi. Twakusihi sana Yesu Mwokozi, Tubatize upya, kwa Roho leo. 2. Kwako twalia, wenye maovu,  Osha moyo wetu, ututakase. 3. Kipaji cha juu, kitume kwetu,  Tubariki sasa, utufariji. 4. Isikilize, kwa moyo wazi,  Sauti ya Roho; ubarikiwe. (Amina)

190 - Raha Yangu Yote, Bwana

190 - Raha Yangu Yote, Bwana "Forever Here My Rest Shall Be" 1. Raha yangu yote, Bwana, I mbavuni pako;  Mimi sina haja tena ila kifo chako. 2. Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu,  Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu. 3. Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu;  Nioshe damuni mwako liwe fungu langu. 4. Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo,  Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo, 5. Na iwe kafara damu nifanyapo kazi,  Hata imani itimu, nikwone,Mwokozi.   (Amina)

191 - Mkate Wa Mbingu

191 - Mkate Wa Mbingu "Break thou The Bread Of Life" 1. Mkate wa mbingu mega kwetu; Ulivyotoa kwa thenashara.  Katika kitabu, twakuona.  Moyo unatweta kukutana. 2. Neno la ukweli libariki;  Tusikie mwito wa upole.  Vizuizi vyote vitakoma.  Tena tutapata uungwana. 3. Uzima na nguvu, utanena;  Nakimbiliza tu kufuata.  Lakini mnyonge ndiye mimi;  Naye Mshindaji ndiye wewe!    (Amina)

192 - Mwamba Wenye Imara

192 - Mwamba Wenye Imara "Rock Of Ages" 1. Mwamba wenye imara,kwako nitajificha! Maji hayo na damu yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi,Hunifanya m-shindi. 2. Kwa kazi zote pia sitimizi sheria, Nijapofanya bidii,nikilia na kudhii, Hayaishi makosa;ndiwe wa kuokoa. 3. Sina cha mkononi,naja msalambani, Nili tupu,nivike;ni mnyonge,nishike; Nili mchafu,naja,nioshe nisijafa. 4. Nikungojapo chini,na kwenda kaburini, Nipaapo mbinguni na kukwona enzini, Roho yangu na iwe rahani mwako wewe (Amina)

193 - Sauti Yake Mchungaji

193 - Sauti Yake Mchungaji            "Hark" 1. Sauti ya Mchungaji, ninasikia jangwani,  Kondoo waliopotea anwaita warudi. Leteni, leteni, leteni toka dhambini;  Leteni, leteni, waleteni kwa Yesu. 2. Nani atakeyekwenda amsaidie Mchungaji,  Awarudishe zizini, wasife bure gizani? 3. Usikose kusikis sauti ya Mchungaji,  "Kondoo waliopotea nwnda na kuwatafuta."   (Amina)

194 - Twaomba Baraka Zako

 194 - Twaomba Baraka Zako 1. Twaomba, Bwana, umpokee Kama mhudumu;  Ambaye anjitoa Kuwa mtumishi. 2. Twaomba, Bwana, umpokee Kama mhudumu;  Neno lako alitoe, Mwangaza kung`aa. 3. Mwokozi wetu, twaomba, na umwandikie  Kitabuni mwako juu Mjumbe wa injili. 4. Silaha zake apewe Kumshinda adui;  Vitabuni awe hohari, Mpaka mauti. 5. Yeye ashindaye, Bwana, Kwa rehema yako,  Ile taji ya dhahabu, Nawe utampa (Amina)

195 - Msingi Wa Kanisa

195 - Msingi Wa Kanisa "The Church Has One Foundation" 1. Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana; Kiumbe chake kipya Akipenda sana;  Kutaka ‘kitafuta Alishuka chini,  Naye kwa haja yake, Akafa Mtini. 2. Lina kila kabila Kisha ndiyo moja  Wokovu wake una Mwokozi ndiyo moja;  Uzazi ni umoja. Moja tumaini.  Chakula ni kimoja. Moja tumaini. 3. Watu hustaajabu Kwa mashaka yote.  Yaipatayo nje Hata ndani mwote;  Ila watakatifu Humwomba, wakikesha   Usiku ni kilio. Asubuhi raha. 4. Mashaka na taabu Hata vita vyake.  Vyangoja matimizo Ya amani yake.  Ndipo kwa macho yetu Twone utukufu  Kanisa ya kushinda itastarehe juu.   (Amina)